Surat Muhammad, aya 23

47:23

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُ فَأَصَمَّهُمۡ وَأَعۡمَىٰٓ أَبۡصَٰرَهُمۡ ٢٣

Ulā'ikal-ladhīna la'anahumullāhu fa asammahum wa a'mā absārahum

Hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao. 23

Maelezo ya chini

23 Hao ndio alio watenga mbali kabisa Mwenyezi Mungu na rehema yake, na akawatia uziwi wasiisikie Haki, na akawatia upofu wa macho wasiione Njia ya Uwongofu.