Surat Muhammad, aya 12

47:12

إِنَّ ٱللَّهَ يُدۡخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يَتَمَتَّعُونَ وَيَأۡكُلُونَ كَمَا تَأۡكُلُ ٱلۡأَنۡعَٰمُ وَٱلنَّارُ مَثۡوٗى لَّهُمۡ ١٢

Innallāha yudkhilul-ladhīna āmanū wa'amilus-sālihāti jannātin tajrī min tahtihal-anhāru walladhīna kafarū yatamatta'ūna waya'kulūna kamā ta'kulul-an'āmu wan-nāru mathwal lahum

Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitiwazo na mito kati yake. Na walio kufuru hujifurahisha na hula kama walavyo wanyama, na Moto ndio makaazi yao. 12

Maelezo ya chini

12 Hakika Mwenyezi Mungu atawatia wenye kuamini na wakatenda mema katika Pepo tukufu zenye kupitiwa ndani yake mito. Na makafiri wanastarehe duniani kidogo, na wanakula kama walavyo wanyama, wamepigwa na mghafala wala hawajifikirii mwisho wao. Hawanalo lao ila matamanio yao. Na kesho Akhera nyumba yao ni Motoni.