Surat Luqman, aya 20

31:20

أَلَمۡ تَرَوۡاْ أَنَّ ٱللَّهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَأَسۡبَغَ عَلَيۡكُمۡ نِعَمَهُۥ ظَٰهِرَةٗ وَبَاطِنَةٗۗ وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِي ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَلَا هُدٗى وَلَا كِتَٰبٖ مُّنِيرٖ ٢٠

Alam taraw annallāha sakkhara lakum mā fis-samāwāti wamā fil-ardi wa asbagha 'alaykum ni'amahū zāhiratan wabātinatan waminan-nāsi man yujādilu fillāhi bighayri 'ilmin walā hudan walā kitābim munīr

Kwani hamwoni ya kwamba Mwenyezi Mungu amevifanya vikutumikieni viliomo mbinguni na kwenye ardhi, na akakujalizieni neema zake, za dhaahiri na za siri? Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu pasipo ilimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru. 20

Maelezo ya chini

20 Mmeona kwamba Mwenyezi Mungu amekudhalilishieni viliomo mbinguni kama jua, na mwezi, na nyota na vyenginevyo; na viliomo katika ardhi, kama mito, na matunda, na wanyama. Naye amekutimizieni neema zake zilio dhaahiri na zilio sitirika, msizo ziona. Na miongoni mwa watu, wapo wanao jadiliana juu ya dhati ya Mwenyezi Mungu na sifa zake bila ya dalili wala uwongozi ulio pokewa kutokana na Nabii au Wahyi (ufunuo) wenye kumurika kwa mwangaza njia ya Haki.