Surat Luqman, aya 12

31:12

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا لُقۡمَٰنَ ٱلۡحِكۡمَةَ أَنِ ٱشۡكُرۡ لِلَّهِۚ وَمَن يَشۡكُرۡ فَإِنَّمَا يَشۡكُرُ لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٞ ١٢

Walaqad ātaynā luqmānal-hikmata anishkur lillāhi waman yashkur fa innamā yashkuru linafsihī waman kafara fa innallāha ghaniyyun hamīd

Na tulimpa Luqman hikima, tukamwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu. Na mwenye kushukuru basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na aliye kufuru, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa. 12

Maelezo ya chini

12 Na hakika tulimpa Luqman hikima, na ilimu, na kauli ya kusibu. Tulimwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema aliyo kupa. Na mwenye kushukuru basi hakika huyo anaitafutia kheri nafsi yake. Na mwenye kuzikufuru neema, akazikataa, na asishukuru kwa ajili yake, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuihitaji shukra yake, na Yeye Mwenyezi Mungu ni Mwenye kustahiki sifa zote njema, na ingawa pasiwepo hata mmoja wa kumsifu.