Surat Ibrahim, aya 19

14:19

أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ وَيَأۡتِ بِخَلۡقٖ جَدِيدٖ ١٩

Alam tara annallāha khalaqas-samāwāti wal-arda bil-haqqi in yasha' yudhhibkum waya'ti bikhalqin jadīd

Huoni kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki? Akitaka atakuondoeni na alete viumbe wapya! 19

Maelezo ya chini

19 Ewe unae semezwa! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi zisimame juu ya Haki kwa mujibu wa hikima yake? Na Mwenye kuweza haya basi anaweza kukuteketezeni, enyi makafiri, na akitaka akaleta viumbe wengine badala yenu nyinyi, ambao watakubali kuwepo kwake, na kwamba Yeye ni Mmoja wa pekee.