وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِرُسُلِهِمۡ لَنُخۡرِجَنَّكُم مِّنۡ أَرۡضِنَآ أَوۡ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَاۖ فَأَوۡحَىٰٓ إِلَيۡهِمۡ رَبُّهُمۡ لَنُهۡلِكَنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ ١٣
Waqālal-ladhīna kafarū lirusulihim lanukhrijannakum min ardinā aw lata'ūdunna fī millatinā fa awhā ilayhim rabbuhum lanuhlikannaz-zālimīn
Na walio kufuru wakawaambia Mitume wao: Tutakutoeni katika nchi yetu, au mrudi katika mila yetu. Basi Mola wao Mlezi aliwaletea wahyi: Hakika tutawaangamiza walio dhulumu. 13
Maelezo ya chini
13 Wakuu wa makafiri majabari wenye madaraka wakaazimia watumie nguvu walipo shindwa wote kupambana kwa hoja na dalili. Wakawaambia Mitume wao: Na liwe moja ya mawili. Ama tukutoeni katika nchi yetu, au muingie katika dini yetu. Mwenyezi Mungu akawafunulia Mitume kwa wahyi: Tutawateketeza hao makafiri kwa dhulma yao!