فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا صَٰلِحٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَمِنۡ خِزۡيِ يَوۡمِئِذٍۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡقَوِيُّ ٱلۡعَزِيزُ ٦٦
Falammā jā'a amrunā najjaynā sālihan walladhīna āmanū ma'ahū birahmatim minnā wamin khizyi yawmi'idhin inna rabbaka huwal-qawiyyul-'azīz
Basi ilipo kuja amri yetu tulimwokoa Swaleh na wale walio amini pamoja naye kwa rehema yetu kutokana na hizaya ya siku ile. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kushinda. 66
Maelezo ya chini
66 Ilipo kuja adhabu yetu tulimwokoa Swaleh na wale walio amini pamoja naye kutokana na maangamizo kwa rehema iliyo toka kwetu khasa. Na tukawaokoa na hizaya na fedheha ya siku ya maangamizo ya Thamud. Hakika Mola wako Mlezi, ewe Nabii, ni Mwenye nguvu na Mwenye kushinda. Basi tuwa ukitegemea nguvu zake, na ushindi wake, na msaada wake, na nusra yake.