فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُواْ فِي دَارِكُمۡ ثَلَٰثَةَ أَيَّامٖۖ ذَٰلِكَ وَعۡدٌ غَيۡرُ مَكۡذُوبٖ ٦٥
Fa'aqarūhā faqāla tamatta'ū fī dārikum thalāthata ayyāmin dhālika wa'dun ghayru makdhūb
Wakamchinja. Basi (Swaleh) akasema: Stareheni katika mji wenu muda wa siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo kuwa ya uwongo. 65
Maelezo ya chini
65 Na wao wasiisikie nasaha yake, wala wasimkubalie. Kiburi chao na dharau yao iliwapelekea kumuuwa yule ngamia. Basi yeye akawaambia: Stareheni na maisha yenu ya kilimwengu katika miji yenu muda wa siku tatu. Kisha baadae itakujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ni ahadi ya kweli wala haina kinyume, wala haina uwongo ndani yake.