وَلَا يَنفَعُكُمۡ نُصۡحِيٓ إِنۡ أَرَدتُّ أَنۡ أَنصَحَ لَكُمۡ إِن كَانَ ٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يُغۡوِيَكُمۡۚ هُوَ رَبُّكُمۡ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ٣٤
Walā yanfa'ukum nushī in arattu an ansaha lakum in kānallāhu yurīdu an yughwiyakum huwa rabbukum wa ilayhi turja'ūn
Wala nasaha yangu haikufaini kitu nikitaka kukunasihini, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kukuachieni mpotee. Yeye ndiye Mola wenu Mlezi; na kwake mtarejeshwa. 34
Maelezo ya chini
34 Wala nasaha yangu haitakufaeni kitu kwa kuwa tu nakutakieni kheri, ikiwa Mwenyezi Mungu anakutakeni mpotee kwa mujibu wa ilimu yake na uwezo wake kwa kuharibika nyoyo zenu, hata zimekuwa haziikubali Haki! Yeye Subhanahu ndiye Mola wenu Mlezi, naye atakurejesheni kwake Siku ya Kiyama. Na atakulipeni kwa mlivyo kuwa mkitenda.