قَالَ إِنَّمَا يَأۡتِيكُم بِهِ ٱللَّهُ إِن شَآءَ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ ٣٣
Qāla innamā ya'tīkum bihillāhu in shā'a wamā antum bimu'jizīn
Akasema (Nuhu) : Mwenyezi Mungu atakuleteeni akipenda, wala nyinyi siwenye kumshinda. 33
Maelezo ya chini
33 Nuhu akasema: Mambo haya yamo mikononi mwa Mwenyezi Mungu pekee. Yeye ndiye atakuleteeni alitakalo kwa hikima yake. Wala nyinyi hamwezi kuikimbia adhabu yake itakapo kuja. Kwani Yeye, Subhanahu, haemewi na chochote katika ardhi wala katika mbingu.