قَالُواْ يَٰنُوحُ قَدۡ جَٰدَلۡتَنَا فَأَكۡثَرۡتَ جِدَٰلَنَا فَأۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ ٣٢
Qālū yānūhu qad jādaltanā fa aktharta jidālanā fa tinā bimā ta'idunā in kunta minas-sādiqīn
Wakasema: Ewe Nuhu! Umejadiliana, na umekithirisha kutujadili. Basi tuletee hayo unayo tuahidi, ukiwa miongoni mwa wasemao kweli. 32
Maelezo ya chini
32 Wakasema: Ewe Nuhu! Umebishana nasi ili tukuamini, na umezidisha kutujadili mpaka tumechoka. Sasa hatuyastahamilii tena maneno yako. Basi, hebu, tuletee hiyo adhabu unayo tutishia, kama wewe kweli unayo yasema kwamba Mwenyezi Mungu atatuadhibu tukito kuamini!