وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦٓ إِنِّي لَكُمۡ نَذِيرٞ مُّبِينٌ ٢٥
Walaqad arsalnā nūhan ilā qawmihī innī lakum nadhīrum mubīn
Na Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akawaambia: Hakika mimi ni mwonyaji kwenu ninaye bainisha, 25
Maelezo ya chini
25 Na kama tulivyo kutuma kwa watu wako uwaonye na uwabashirie kheri, wakakukabili baadhi yao kwa inadi na upinzani, kadhaalika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akawaambia: Mimi nakuhadharisheni na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na nakuonyesheni njia ya kuokoka.