Surat Hud, aya 26

11:26

أَن لَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۖ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ أَلِيمٖ ٢٦

Al lā ta'budū illallāha innī akhāfu 'alaykum 'adhāba yawmin alīm

Ya kwamba msimuabudu isipo kuwa Mwenyezi Mungu tu. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Chungu. 26

Maelezo ya chini

26 Akawaambia: Mimi nilitakalo kwenu ni kuwa msimuabudu ila Mwenyezi Mungu tu, kwa sababu nakukhofieni, mkimuabudu mwenginewe au mkimshirikisha pamoja naye wenginewe katika kumuabudu, isije ikakufikieni siku ya adhabu yake yenye machungu makali.