Surat Hud, aya 123

11:123

وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَإِلَيۡهِ يُرۡجَعُ ٱلۡأَمۡرُ كُلُّهُۥ فَٱعۡبُدۡهُ وَتَوَكَّلۡ عَلَيۡهِۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ ١٢٣

Walillāhi ghaybus-samāwāti wal-ardi wa ilayhi yurja'ul-amru kulluhū fa'budhu watawakkal 'alayhi wamā rabbuka bighāfilin 'ammā ta'malūn

Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyo fichikana katika ardhi na mbingu, na mambo yote yatarejezwa kwake. Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye. Na Mola wako Mlezi haghafiliki na yale mnayo yatenda. 123

Maelezo ya chini

123 Ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kujua yaliyo ya ghaibu katika mbingu na ardhi. Anayajua yatakayo kufikieni, na yatakayo tufikia sisi. Ni kwake Yeye tu yanarejea mambo yote kuendeshwa. Ilivyo kuwa mambo ni hivyo, basi muabudu Mola wako Mlezi peke yake, na mtegemee Yeye, wala usimwogope yeyote isipo kuwa Yeye. Na Mola wako Mlezi haghafiliki kabisa na yote myatendayo, enyi Waumini na makafiri. Na kila mmoja atalipwa hapa duniani na Akhera kwa mujibu anavyo stahiki.