Hasbunallahu wa ni'mal wakil

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

ٱلَّذِينَ قَالَ لَهُمُ ٱلنَّاسُ إِنَّ ٱلنَّاسَ قَدۡ جَمَعُواْ لَكُمۡ فَٱخۡشَوۡهُمۡ فَزَادَهُمۡ إِيمَٰنٗا وَقَالُواْ حَسۡبُنَا ٱللَّهُ وَنِعۡمَ ٱلۡوَكِيلُ ١٧٣

Alladhīna qāla lahumun-nāsu innan-nāsa qad jama'ū lakum fakhshawhum fazādahum īmānan waqālū hasbunallāhu wani'mal-wakīl

Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa. 173

Maelezo ya chini

173 Hao ndio walio tiwa khofu na watu kwa kuwaambia: Maadui zenu wamekusanya jeshi kubwa kukupigeni, basi waogopeni. Na wao hawakudhoofika wala hawakulegea, bali walizidi Imani ya Mwenyezi Mungu na wakawa na moyo kuwa atawanusuru. Jawabu yao ikawa: Mwenyezi Mungu anatutosheleza. Yeye ndiye aliye tawala mambo yetu. Na Yeye ndiye anaye tegemezwa mambo yote.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Al-Imran yote

Maswali

Hasbunallahu wa ni'mal wakil iko wapi katika Qur'ani?

Hasbunallahu wa ni'mal wakil iko katika Surat Al-Imran, 3:173.