نَحۡنُ أَوۡلِيَآؤُكُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۖ وَلَكُمۡ فِيهَا مَا تَشۡتَهِيٓ أَنفُسُكُمۡ وَلَكُمۡ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ ٣١
Nahnu awliyā'ukum fil-hayawātid-dunyā wafil-ākhirati walakum fīhā mā tashtahī anfusukum walakum fīhā mā tadda'ūn
Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinacho tamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyo vitaka. 31
Maelezo ya chini
31 Na Malaika watawaambia: Sisi ni wasaidizi wenu katika maisha ya duniani kwa kukuungeni mkono, na Akhera kwa kukuombeeni shafaa na kukutukuzeni. Na huko Akhera mtapata kila cha ladha na kizuri kinacho pendwa na nafsi zenu, na mtapata kila mnacho kitamani kuwa ni takrima, na maamkio yanayo toka kwa Mola Mlezi Mkunjufu wa maghfira na rehema.