Surat Fussilat, aya 32

41:32

نُزُلٗا مِّنۡ غَفُورٖ رَّحِيمٖ ٣٢

Nuzulam min ghafūrir rahīm

Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 32

Maelezo ya chini

32 Na Malaika watawaambia: Sisi ni wasaidizi wenu katika maisha ya duniani kwa kukuungeni mkono, na Akhera kwa kukuombeeni shafaa na kukutukuzeni. Na huko Akhera mtapata kila cha ladha na kizuri kinacho pendwa na nafsi zenu, na mtapata kila mnacho kitamani kuwa ni takrima, na maamkio yanayo toka kwa Mola Mlezi Mkunjufu wa maghfira na rehema.