Surat Fussilat, aya 3

41:3

كِتَٰبٞ فُصِّلَتۡ ءَايَٰتُهُۥ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا لِّقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ ٣

Kitābun fussilat āyātuhū qur'ānan 'arabiyyal liqawmin ya'lamūn

Hichi ni Kitabu kilicho pambanuliwa Aya zake, cha kusomwa kwa Kiarabu kwa watu wanao jua. 3

Maelezo ya chini

3 Kitabu hichi ni namna ya peke yake kwa uzuri wake kwa matamshi na ibara yake ya utungaji, na kwa maana inavyo pambanua baina Haki na baat'ili, na bishara na onyo, na kuzitengeneza nafsi, na kupiga mifano, na kubainisha hukumu. Nacho kinasomwa kwa ulimi wa Kiarabu, chepesi kukifahamu kwa watu wanao jua.