وَٱللَّهُ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ ٱلرِّيَٰحَ فَتُثِيرُ سَحَابٗا فَسُقۡنَٰهُ إِلَىٰ بَلَدٖ مَّيِّتٖ فَأَحۡيَيۡنَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَاۚ كَذَٰلِكَ ٱلنُّشُورُ ٩
Wallāhul-ladhī arsalar-riyāha fatuthīru sahāban fasuqnāhu ilā baladim mayyitin fa ahyaynā bihil-arda ba'da mawtihā kadhālikan-nushūr
Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye zituma Pepo ziyatimue mawingu, nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyo kufa, tukaifufua ardhi baada ya kufa kwake. Ndivyo kama hivyo kutakavyo kuwa kufufuliwa. 9
Maelezo ya chini
9 Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anaye zituma pepo ziyatimue mawingu yaliyo rindika kwa mvuke wa maji. Tena tukayasukuma hayo mawingu mpaka kwenye nchi yenye ukame, tukaihuisha ardhi yake baada ya kuwa ilikuwa imekufa. Kama tunavyo itoa mimea katika ardhi, basi hali kadhaalika tutawatoa maiti makaburini Siku ya Kiyama. Rejea maoni ya ki-ilimu juu ya Aya 57 katika Surat Al Aa'raaf.