Surat Fatir, aya 42

35:42

وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَئِن جَآءَهُمۡ نَذِيرٞ لَّيَكُونُنَّ أَهۡدَىٰ مِنۡ إِحۡدَى ٱلۡأُمَمِۖ فَلَمَّا جَآءَهُمۡ نَذِيرٞ مَّا زَادَهُمۡ إِلَّا نُفُورًا ٤٢

Wa aqsamū billāhi jahda aymānihim la in jā'ahum nadhīrul layakūnunna ahdā min ihdal-umami falammā jā'ahum nadhīrum mā zādahum illā nufūrā

Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa kuapa kwao, kwamba akiwajia mwonyaji bila ya shaka watakuwa waongofu zaidi kuliko taifa jingine lolote. Lakini alipo wajia mwonyaji hakuwazidishia ila kuikimbia hiyo Haki, 42

Maelezo ya chini

42 Na makafiri waliapa kwa jina la Mwenyezi Mungu mwisho wa juhudi yao kutilia nguvu kiapo chao, ya kwamba bila ya shaka akiwajia Mtume kuwaonya basi wao hapana shaka watakuwa miongoni mwa mataifa walio ongoka zaidi kuliko hao wenginewe walio wakadhibisha Mitume wao. Lakini alipo wajia Mtume kutokana na wao wenyewe, akiwaonya, hakuwazidishia kwa kuwaonya kwake na kuwanasihi, isipo kuwa kuikimbia Haki.