Surat Fatir, aya 24

35:24

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗاۚ وَإِن مِّنۡ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٞ ٢٤

Innā arsalnāka bil-haqqi bashīran wanadhīran wa im min ummatin illā khalā fīhā nadhīr

Hakika Sisi tumekutuma wewe kwa Haki, kuwa ni mbashiri na mwonyaji. Na hapana umma wowote ila ulipata mwonyaji kati yao. 24

Maelezo ya chini

24 Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma wewe uwafikishie watu wote hii Dini ya Haki, ukiwabashiria Pepo wenye kuamini, na ukiwaonya kwa adhabu ya Moto wanao ikataa hii Dini. Na hapana kaumu yoyote katika kaumu zilizo pita ila walijiwa na mtu kutokana na Mwenyezi Mungu wa kuwahadharisha na adhabu yake.