Surat Fatir, aya 14

35:14

إِن تَدۡعُوهُمۡ لَا يَسۡمَعُواْ دُعَآءَكُمۡ وَلَوۡ سَمِعُواْ مَا ٱسۡتَجَابُواْ لَكُمۡۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَكۡفُرُونَ بِشِرۡكِكُمۡۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثۡلُ خَبِيرٖ ١٤

In tad'ūhum lā yasma'ū du'ā'akum walaw sami'ū mastajābū lakum wayawmal-qiyāmati yakfurūna bishirkikum walā yunabbi'uka mithlu khabīr

Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakaye kupa khabari vilivyo kama Yeye Mwenye khabari. 14

Maelezo ya chini

14 Mkiwaomba hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawasikii maombi yenu. Na hata ingeli kuwa wanasikia wasingeli kujibuni kitu chochote kwa hayo myatakayo. Na Siku ya Kiyama watakuja kukataa huo ushirikina wenu kuwashirikisha na Mwenyezi Mungu. Wala hapana wa kukupeni khabari za hali za Akhera kuliko huyo Mwenye kuzijua vyema kwa ujuzi wa ndani kabisa.