Surat Az-Zumar, aya 73

39:73

وَسِيقَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ رَبَّهُمۡ إِلَى ٱلۡجَنَّةِ زُمَرًاۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُوهَا وَفُتِحَتۡ أَبۡوَٰبُهَا وَقَالَ لَهُمۡ خَزَنَتُهَا سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡ طِبۡتُمۡ فَٱدۡخُلُوهَا خَٰلِدِينَ ٧٣

Wasīqal-ladhīnat-taqaw rabbahum ilal-jannati zumaran hattā idhā jā'ūhā wafutihat abwābuhā waqāla lahum khazanatuhā salāmun 'alaykum tibtum fadkhulūhā khālidīn

Na walio mcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa makundi, mpaka watakapo fikilia, nayo milango yake imekwisha funguliwa. Walinzi wake watawaambia: Salaam Alaikum, Amani iwe juu yenu! Mmet'ahirika. Basi ingieni humu mkae milele. 73

Maelezo ya chini

73 Na wachamngu watahimizwa kwenda Peponi kwa hishima makundi makundi, mpaka wakifika kwenye milango yake, wataambiwa na walinzi wake: Amani kubwa juu yenu! Mmet'ahirika duniani na uchafu wa maasi, na mmet'ahirika Akhera katika nafsi zenu kwa neema mlizo zipata. Basi ingieni Peponi mliko jaaliwa kukaa milele. Kwani nyinyi mna neema zisio pita akilini.