۞ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَذَبَ عَلَى ٱللَّهِ وَكَذَّبَ بِٱلصِّدۡقِ إِذۡ جَآءَهُۥٓۚ أَلَيۡسَ فِي جَهَنَّمَ مَثۡوٗى لِّلۡكَٰفِرِينَ ٣٢
Faman azlamu mimman kadhaba 'alallāhi wakaddhaba bis-sidqi idh jā'ahū alaysa fī jahannama mathwal lil-kāfirīn
BASI NI NANI dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye msingizia uwongo Mwenyezi Mungu na kuikanusha kweli imfikiapo? Je! Siyo katika Jahannamu makaazi ya hao makafiri? 32
Maelezo ya chini
32 Basi hapana aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye msingizia Mwenyezi Mungu lisio kuwa lake, na akaikanusha Haki bila ya kufikiri wala kuzingatia pale inapo mjia kwa ndimi za Mitume. Kwani katika Jahannamu sio makaazi ya makafiri walio ghurika hata wakamfanyia jeuri Mwenyezi Mungu?