Surat Az-Zukhruf, aya 87

43:87

وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَهُمۡ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۖ فَأَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ ٨٧

Wala'in sa'altahum man khalaqahum layaqūlunnallāhu fa annā yu'fakūn

Na ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanako geuziwa? 87

Maelezo ya chini

87 Na ewe Mtume! Ukiwauliza hawa washirikina nani aliye waumba, bila ya shaka watasema: Kawaumba Mwenyezi Mungu. Basi inakuwaje wakaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu wakenda kuwaabudu wenginewe, nao wanakiri kuwa Yeye ndiye Muumba wao? Ama hakika jambo hili ni la ajabu!