Surat Az-Zukhruf, aya 76

43:76

وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن كَانُواْ هُمُ ٱلظَّٰلِمِينَ ٧٦

Wamā zalamnāhum walākin kānū humuz-zālimīn

Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio walio kuwa madhaalimu. 76

Maelezo ya chini

76 Wala Sisi hatukuwadhulumu wakosefu hawa kwa adhabu hii, lakini wao wenyewe ndio walio jidhulumu nafsi zao kwa kukhiari upotofu kuliko uwongofu.