يُطَافُ عَلَيۡهِم بِصِحَافٖ مِّن ذَهَبٖ وَأَكۡوَابٖۖ وَفِيهَا مَا تَشۡتَهِيهِ ٱلۡأَنفُسُ وَتَلَذُّ ٱلۡأَعۡيُنُۖ وَأَنتُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ٧١
Yutāfu 'alayhim bisihāfim min dhahabin wa akwābin wafīhā mā tashtahīhil-anfusu wataladdhul-a'yunu wa antum fīhā khālidūn
Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele. 71
Maelezo ya chini
71 Na baada ya kuingia Peponi watakuwa wakizungukiwa kwa sahani za dhahabu, na bilauri kadhaalika, na humo watapata vyakula namna mbali mbali, na vinywaji vya kila namna. Na humo Peponi watapata kila kitamaniacho moyo, na kituzacho macho. Na kukamilisha furaha wataambiwa: Nyinyi mtakaa milele katika neema hizi.