حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَنَا قَالَ يَٰلَيۡتَ بَيۡنِي وَبَيۡنَكَ بُعۡدَ ٱلۡمَشۡرِقَيۡنِ فَبِئۡسَ ٱلۡقَرِينُ ٣٨
Hattā idhā jā'anā qāla yālayta baynī wabaynaka bu'dal-mashriqayni fabi'sal-qarīn
Hata atakapo tujia atasema: Laiti ungeli kuwako baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe! 38
Maelezo ya chini
38 Hata yule aliye jipa upofu na Qur'ani atapo fika kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, na akaona matokeo ya kule kujitia kwake upofu, atamwambia rafiki yake kwa majuto: Laiti wewe nami tungeli kuwa mbali mbali duniani umbali wa mashariki na magharibi! Ama wewe ulikuwa sahibu muovu mno kwangu, mpaka umekuja nitumbukize katika shimo la Motoni!