أَمۡ عِندَهُمۡ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمۡ هُمُ ٱلۡمُصَۜيۡطِرُونَ ٣٧
Am 'indahum khazā'inu rabbika am humul-musaytirūn
Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka? 37
Maelezo ya chini
37 Kwani wao wanazo khazina za Mola wako Mlezi wanazo zisarifu watakavyo? Au wana nguvu za kutenda watakavyo, na kupanga mambo kama wapendavyo?