Surat At-Tawbah, aya 94

9:94

يَعۡتَذِرُونَ إِلَيۡكُمۡ إِذَا رَجَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡۚ قُل لَّا تَعۡتَذِرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكُمۡ قَدۡ نَبَّأَنَا ٱللَّهُ مِنۡ أَخۡبَارِكُمۡۚ وَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ٩٤

Ya'tadhirūna ilaykum idhā raja'tum ilayhim qul lā ta'tadhirū lan nu'mina lakum qad nabba'anallāhu min akhbārikum wasayarallāhu 'amalakum warasūluhū thumma turaddūna ilā 'ālimil-ghaybi wash-shahādati fayunabbi'ukum bimā kuntum ta'malūn

WATAKUTOLEENI UDHURU mtapo warudia. Sema: Msitoe udhuru; hatukuaminini. Mwenyezi Mungu amekwisha tueleza khabari zenu. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ya siri na ya dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda. 94

Maelezo ya chini

94 Enyi Waumini Mujaahidina! Hao walio bakia nyuma na wakafanya taksiri watakutoleeni udhuru mtapo rejea kutoka vitani na mkakutana nao. Ewe Mtume! Waambie: Msitoe udhuru, kwani hakika sisi hatukusadikini. Mwenyezi Mungu amekwisha bainisha wazi ukweli wa roho zenu, na amemfunulia Nabii wake baadhi ya uwongo wenu. Na baada ya hayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake watavijua vitendo vyenu. Na mwisho wenu baada ya maisha ya duniani ni kuendea kwa Mwenyezi Mungu ambaye anayajua yaliyo fichikana na yanayo onekana wazi. Naye atakulipeni kwa mliyo kuwa mkiyatenda. Na atakulipeni kwa mnavyo stahiki.