Surat At-Tawbah, aya 83

9:83

فَإِن رَّجَعَكَ ٱللَّهُ إِلَىٰ طَآئِفَةٖ مِّنۡهُمۡ فَٱسۡتَـٔۡذَنُوكَ لِلۡخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخۡرُجُواْ مَعِيَ أَبَدٗا وَلَن تُقَٰتِلُواْ مَعِيَ عَدُوًّاۖ إِنَّكُمۡ رَضِيتُم بِٱلۡقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٖ فَٱقۡعُدُواْ مَعَ ٱلۡخَٰلِفِينَ ٨٣

Fa ir raja'akallāhu ilā tā'ifatim minhum fasta'dhanūka lil-khurūji faqul lan takhrujū ma'iya abadan walan tuqātilū ma'iya 'aduwwan innakum radītum bil-qu'ūdi awwala marratin faq'udū ma'al-khālifīn

Basi Mwenyezi Mungu akikurudisha kwenye kikundi kimoja miongoni mwao - na wakakutaka idhini ya kutoka - sema: Nyinyi hamtatoka pamoja nami kabisa, wala hamtapigana na adui pamoja nami. Nyinyi mliridhia kukaa nyuma mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na hao watakao bakia nyuma. 83

Maelezo ya chini

83 Ukirejea kutoka vitani wakawa baadhi ya hawa wanaafiki walio kataa kwenda vitani wakakutaka ruhusa watoke nawe kwenda Jihadi katika vita vingine, basi wewe usiwakubalie, na waambie: Hamtokwenda nami katika vita vyo vyote, wala hamtoshirikiana nami katika kupigana kokote na adui. Kwani kukaa kwenu nyuma msitoke pale mara ya kwanza hakukuwa na udhuru wowote unao faa, wala haikutokea toba yoyote ya kustahiki msamaha! Basi kaeni kama mlivyo ridhia kukaa pamoja na wazee na wakongwe na wanawake na watoto wadogo walio bakia nyuma.