فَرِحَ ٱلۡمُخَلَّفُونَ بِمَقۡعَدِهِمۡ خِلَٰفَ رَسُولِ ٱللَّهِ وَكَرِهُوٓاْ أَن يُجَٰهِدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَالُواْ لَا تَنفِرُواْ فِي ٱلۡحَرِّۗ قُلۡ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرّٗاۚ لَّوۡ كَانُواْ يَفۡقَهُونَ ٨١
Farihal-mukhallafūna bimaq'adihim khilāfa rasūlillāhi wakarihū an yujāhidū bi amwālihim wa anfusihim fī sabīlillāhi waqālū lā tanfirū fil-harri qul nāru jahannama ashaddu harral law kānū yafqahūn
Walifurahi walio achwa nyuma kwa kule kubakia kwao nyuma na kumuacha Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walichukia kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao, na wakasema: Msitoke nje katika joto! Sema: Moto wa Jahannamu una joto zaidi, laiti wangeli fahamu! 81
Maelezo ya chini
81 Hakika wanaafiki walibaki nyuma wasitoke pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenda kuwakaabili maadui, na wakafurahi kubakia Madina baada ya kutoka Nabii, na kukhalifu amri yake ya kwenda kwenye Jihadi. Walichukia kutumia mali yao na kujitolea roho zao kwa ajili ya Jihadi kulinyanyua Neno la Mwenyezi Mungu na kuinusuru Dini yake. Wakawa wao wakiwavunja moyo wengineo, na wakiwashawishi wabaki nyuma pamoja nao, na wakiwatisha wasende vitani katika joto kama hilo! Ewe Mtume! Waambie hawa: Kama nyinyi mna akili mtakumbuka kuwa vukuto la Moto wa Jahannamu ni kali zaidi na lina shida zaidi kuliko hili mnalo likhofu.