كَيۡفَ وَإِن يَظۡهَرُواْ عَلَيۡكُمۡ لَا يَرۡقُبُواْ فِيكُمۡ إِلّٗا وَلَا ذِمَّةٗۚ يُرۡضُونَكُم بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَتَأۡبَىٰ قُلُوبُهُمۡ وَأَكۡثَرُهُمۡ فَٰسِقُونَ ٨
Kayfa wa in yazharū 'alaykum lā yarqubū fīkum illan walā dhimmatan yurdūnakum bi afwāhihim wata'bā qulūbuhum wa aktharuhum fāsiqūn
Itakuwaje! Nao wakikushindeni hawatazami kwenu udugu wala ahadi. Wanakufurahisheni kwa midomo yao tu, na nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wapotovu. 8
Maelezo ya chini
8 Vipi nyinyi mtalinda ahadi zao nao ni watu ambao wakikuwezeni wanawasaidia maadui zenu dhidi yenu? Hawataacha fursa ya kukumalizeni bila ya kujali ujamaa (udugu) wala mapatano. Na watu hao hukudanganyeni kwa maneno yao yaliyo pakwa asali, na nyoyo zao zimekunja kwa kukuchukieni. Na wengi wao wametokana na Haki, ni wenye kuvunja ahadi.