أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ سِرَّهُمۡ وَنَجۡوَىٰهُمۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ عَلَّٰمُ ٱلۡغُيُوبِ ٧٨
Alam ya'lamū annallāha ya'lamu sirrahum wanajwāhum wa annallāha 'allāmul-ghuyūb
Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri zao na minong'ono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua sana ya ghaibu? 78
Maelezo ya chini
78 Vipi wanajitia ujinga na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema? Hapana chochote wanacho dhamiria kisirisiri katika kuvunja ahadi kinacho fichikana kwake. Wala wanacho kinong'ona kwa uficho katika kuitia kombo Dini na kuwapangia njama Waislamu. Naye, aliye tukuka shani yake, ni Mjuzi mno hapitikiwi na kitu chochote..