Surat At-Tawbah, aya 77

9:77

فَأَعۡقَبَهُمۡ نِفَاقٗا فِي قُلُوبِهِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ يَلۡقَوۡنَهُۥ بِمَآ أَخۡلَفُواْ ٱللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُواْ يَكۡذِبُونَ ٧٧

Fa a'qabahum nifāqan fī qulūbihim ilā yawmi yalqawnahū bimā akhlafullāha mā wa'adūhu wabimā kānū yakdhibūn

Basi akawalipa unaafiki kuutia nyoyoni mwao mpaka Siku watapo kutana naye, kwa sababu ya kuwa walimkhalifu Mwenyezi Mungu katika yale waliyo muahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uwongo. 77

Maelezo ya chini

77 Matokeo ya ubakhili wao ni kujaa unaafiki katika nyoyo zao mpaka watakapo kufa na wakakutana na Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya kuvunja ahadi zao na uwongo wao katika viapo vyao.