ٱلَّذِينَ يَلۡمِزُونَ ٱلۡمُطَّوِّعِينَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ فِي ٱلصَّدَقَٰتِ وَٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهۡدَهُمۡ فَيَسۡخَرُونَ مِنۡهُمۡ سَخِرَ ٱللَّهُ مِنۡهُمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ ٧٩
Alladhīna yalmizūnal-muttawwi'īna minal-mu'minīna fis-sadaqāti walladhīna lā yajidūna illā juhdahum fayaskharūna minhum sakhirallāhu minhum walahum 'adhābun alīm
Wale wanao wabeuwa Waumini wanao toa sadaka nyingi na wasio nacho cha kutoa ila kadri ya juhudi yao, basi huwakejeli. Mwenyezi Mungu atawakejeli wao! Nao watapata adhabu chungu! 79
Maelezo ya chini
79 Na katika ila zao hawa wanaafiki pamoja na ubakhili wao ni kuwa wao huwakejeli Waumini wenye nafasi kwa vile kusabilia mali yao kwa wanao hitajia, na huwafanyia maskhara wale wenye nafasi ndogo wanao toa sadaka juu ya kuwa wenyewe walicho nacho ni kidogo. Mwenyezi Mungu kesha walipa kwa hizo kejeli zao kwa kuwakashifu wakatambulikana fedheha zao, wakawa wao ndio kichekesho cha watu wote. Na kesho Akhera adhabu yao itakuwa kali.