Surat At-Tawbah, aya 65

9:65

وَلَئِن سَأَلۡتَهُمۡ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلۡعَبُۚ قُلۡ أَبِٱللَّهِ وَءَايَٰتِهِۦ وَرَسُولِهِۦ كُنتُمۡ تَسۡتَهۡزِءُونَ ٦٥

Wala'in sa'altahum layaqūlunna innamā kunnā nakhūdu wanal'abu qul abillāhi wa āyātihī warasūlihī kuntum tastahzi'ūn

Na ukiwauliza, wanasema: Sisi tulikuwa tukipiga porojo na kucheza tu. Sema: Mlikuwa mkimfanyia maskhara Mwenyezi Mungu na Ishara zake na Mtume wake? 65

Maelezo ya chini

65 Ewe Mtume! Kuwa na yakini kwamba, baada ya kwisha fedheheka mambo yao hawa wanaafiki, ukawauliza sababu ya kuitia ila Dini na kumfanyia kejeli Mwenyezi Mungu na Ishara zake, wao hutoa udhuru kwa kusema: Tulikuwa tunapiga porojo na tukicheza tu! Waambie: Vipi inakufalieni kupiga porojo na kucheza kwa kumfanyia maskhara Mwenyezi Mungu na Aya zake na Mtume wake?