Surat At-Tawbah, aya 63

9:63

أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّهُۥ مَن يُحَادِدِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَأَنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدٗا فِيهَاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡخِزۡيُ ٱلۡعَظِيمُ ٦٣

Alam ya'lamū annahū man yuhādidillāha warasūlahū fa anna lahū nāra jahannama khālidan fīhā dhālikal-khizyul-'azīm

Je, hawajui ya kwamba anaye shindana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi huyo atapata Moto wa Jahannamu adumu humo? Hiyo ndiyo hizaya kubwa. 63

Maelezo ya chini

63 Hivyo hawa wanaafiki hawajui kwamba malipo ya mwenye kumkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akashindana nao ni adhabu ya daima katika Moto wa Jahannamu? Na hiyo ndiyo hizaya ya kufedhehesha, na madhila makubwa.