يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمۡ لِيُرۡضُوكُمۡ وَٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ أَحَقُّ أَن يُرۡضُوهُ إِن كَانُواْ مُؤۡمِنِينَ ٦٢
Yahlifūna billāhi lakum liyurdūkum wallāhu warasūluhū ahaqqu an yurdūhu in kānū mu'minīn
Wanakuapieni Mwenyezi Mungu ili kukuridhisheni nyinyi, hali ya kuwa wanao stahiki zaidi kuridhishwa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake, lau kama wao ni Waumini. 62
Maelezo ya chini
62 Katika kwenda vitani wao hubaki nyuma hawatoki nanyi kwenda kupigana na adui zenu wala hawataradadi. Na kisha hukutoleeni udhuru wa uwongo kwa kule kubaki kwao nyuma. Na hukuapieni ili muwaridhie na mkubali udhuru wao. Na wa kustahiki kutakiwa radhi kama wao kweli ni Waumini, ni Mwenyezi Mungu na Mtume.