لَقَدِ ٱبۡتَغَوُاْ ٱلۡفِتۡنَةَ مِن قَبۡلُ وَقَلَّبُواْ لَكَ ٱلۡأُمُورَ حَتَّىٰ جَآءَ ٱلۡحَقُّ وَظَهَرَ أَمۡرُ ٱللَّهِ وَهُمۡ كَٰرِهُونَ ٤٨
Laqadibtaghawul-fitnata min qablu waqallabū lakal-umūra hattā jā'al-haqqu wazahara amrullāhi wahum kārihūn
Tangu zamani walitaka kukutilieni fitna, na wakakupindulia mambo juu chini, mpaka ikaja Haki na ikadhihirika amri ya Mwenyezi Mungu, na wao wamechukia. 48
Maelezo ya chini
48 Na hawa wanaafiki walikwisha tangulia kuleta fitna baina yenu, na wewe, ewe Mtume, wakakupangia njama. Lakini Mwenyezi Mungu aliviviza vitimbi vyao, na akahakikisha kukunusuru, na akaipa ushindi Dini yake wao wakipenda wasipende.