لَوۡ خَرَجُواْ فِيكُم مَّا زَادُوكُمۡ إِلَّا خَبَالٗا وَلَأَوۡضَعُواْ خِلَٰلَكُمۡ يَبۡغُونَكُمُ ٱلۡفِتۡنَةَ وَفِيكُمۡ سَمَّٰعُونَ لَهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّٰلِمِينَ ٤٧
Law kharajū fīkum mā zādūkum illā khabālan wala'awda'ū khilālakum yabghūnakumul-fitnata wafīkum sammā'ūna lahum wallāhu 'alīmu biz-zālimīn
Lau wangeli toka nanyi wasingeli kuzidishieni ila mchafuko, na wange tanga tanga kati yenu kukutilieni fitna. Na miongoni mwenu wapo wanao wasikiliza. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu. 47
Maelezo ya chini
47 Na pindi wangeli toka pamoja nanyi wasinge kuzidishieni nguvu zozote. Lakini wao wangeeneza wasiwasi na kuzidisha fitna, na wakaieneza kati yenu. Na miongoni mwenu wapo wasio jua uovu wa niya zao, na huenda pengine wangeli khadaika na maneno yao, na wakazisikiliza fitna zao. Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema hao wanaafiki, wanao jidhulumu nafsi zao kwa ule uharibifu wanao udhamiria.