وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ فَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمۡ زَادَتۡهُ هَٰذِهِۦٓ إِيمَٰنٗاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَزَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَهُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ ١٢٤
Wa idhā mā unzilat sūratun faminhum man yaqūlu ayyukum zādathu hādhihī īmānan fa ammal-ladhīna āmanū fazādathum īmānan wahum yastabshirūn
Na inapo teremshwa Sura wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Ama wale walio amini inawazidishia Imani, nao wanafurahi. 124
Maelezo ya chini
124 Na ikiteremka Sura ya Qur'ani wakaisikia wanaafiki huifanyia maskhara na kuikejeli. Huambizana wao kwa wao: Nani katika nyinyi iliyo mzidisha Imani? Ndio Mwenyezi Mungu anawajibu ya kwamba ipo farka baina ya wanaafiki na Waumini. Ama Waumini ndio wale walio iona Nuru na wakaijua Haki. Hao Aya za Mwenyezi Mungu zimewazidishia Imani, na wao huzifurahia wakati zinapo teremka.