۞ وَمَا كَانَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةٗۚ فَلَوۡلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرۡقَةٖ مِّنۡهُمۡ طَآئِفَةٞ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي ٱلدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوۡمَهُمۡ إِذَا رَجَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَحۡذَرُونَ ١٢٢
Wamā kānal-mu'minūna liyanfirū kāffatan falawlā nafara min kulli firqatim minhum tā'ifatul liyatafaqqahū fid-dīni waliyundhirū qawmahum idhā raja'ū ilayhim la'allahum yahdharūn
Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadharisha?. 122
Maelezo ya chini
122 Haifai Waumini watoke wote kwenda kwa Mtume s.a.w. ila iwe dharura. Itakikanavyo ni kutoka kikundi kwenda kwa Mtume kwa ajili ya kusoma Dini, na wapate kuwaita watu wao kuwaonya na kuwabashiria, pale wanapo rejea. Haya ili wapate kuwa imara daima juu ya Haki, na watahadhari na upotovu na uharibifu.