يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَآ أَحَلَّ ٱللَّهُ لَكَۖ تَبۡتَغِي مَرۡضَاتَ أَزۡوَٰجِكَۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ١
Yā'ayyuhan-nabiyyu lima tuharrimu mā ahallallāhu laka tabtaghī mardāta azwājika wallāhu ghafūrur rahīm
Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alicho kuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 1
Maelezo ya chini
1 Ewe Nabii! Kwa nini unajikhini nafsi yako alicho kuhalalishia Mwenyezi Mungu? Unataka kuwaridhi wakezo, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mkunjufu wa kurehemu.