Surat At-Taghabun, aya 3

64:3

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّ وَصَوَّرَكُمۡ فَأَحۡسَنَ صُوَرَكُمۡۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ ٣

Khalaqas-samāwāti wal-arda bil-haqqi wasawwarakum fa ahsana suwarakum wa ilayhil-masīr

Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura zenu. Na marudio ni kwake. 3

Maelezo ya chini

3 Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa hikima isiyo na ukomo, na akakuumbeni kwa sura, na akazifanya nzuri sura zenu, kwa kuwa amewafanya wanaadamu ndio viumbe walio nyooka vizuri. Na kwake Yeye ndiyo marejeo Siku ya Kiyama.