وَمِنۡ ءَايَٰتِهِۦ خَلۡقُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن دَآبَّةٖۚ وَهُوَ عَلَىٰ جَمۡعِهِمۡ إِذَا يَشَآءُ قَدِيرٞ ٢٩
Wamin āyātihī khalqus-samāwāti wal-ardi wamā battha fīhimā min dābbatin wahuwa 'alā jam'ihim idhā yashā'u qadīr
Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na wanyama alio waeneza. Naye ni Mwenye uweza wa kuwakusanya apendapo. 29
Maelezo ya chini
29 Na katika dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu kuumba atakacho ni huku kuumba mbingu na ardhi kwa nidhamu iliyo pangwa; na kuumbwa vilivyo tenganishwa humo na kuenezwa wanayama wanao onekana na wengineo. Na Mwenyezi Mungu aliye hakikisha uweza wake kwa kuumba hivyo vilio tajwa ni Muweza wa kuwakusanya wote katika wakati autakao kuwafufulia kwa ajili ya malipo.