أَوَلَمۡ يَهۡدِ لَهُمۡ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَبۡلِهِم مِّنَ ٱلۡقُرُونِ يَمۡشُونَ فِي مَسَٰكِنِهِمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٍۚ أَفَلَا يَسۡمَعُونَ ٢٦
Awalam yahdi lahum kam ahlaknā min qablihim minal-qurūni yamshūna fī masākinihim inna fī dhālika la'āyātin afalā yasma'ūn
Je! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii? 26
Maelezo ya chini
26 Je! Kwani Mwenyezi Mungu aliwaacha walio wakadhibisha Mitume wao, na hakuwabainishia kwamba Yeye aliwahilikisha wengi katika kaumu zilizo watangulia, na wao wanapita kwenye majumba yao, na wanatembea kwenye maskani zao? Hakika katika hayo pana mawaidha ya kuwaonyesha Haki. Wao wameingiwa na uziwi, hawasikii mawaidha haya.