أَفَمَن كَانَ مُؤۡمِنٗا كَمَن كَانَ فَاسِقٗاۚ لَّا يَسۡتَوُۥنَ ١٨
Afaman kāna mu'minan kaman kāna fāsiqal lā yastawūn
Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa. 18
Maelezo ya chini
18 Kwani watu watakuwa sawa katika malipo yao, na hali wamekhitalifiana katika vitendo vyao? Je! Aliye kuwa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu ni kama mwenye kumkataa na akamuasi? Hasha! Hawawi sawa!