Surat As-Saffat, aya 68

37:68

ثُمَّ إِنَّ مَرۡجِعَهُمۡ لَإِلَى ٱلۡجَحِيمِ ٦٨

Thumma inna marji'ahum la ilal-jahīm

Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu. 68

Maelezo ya chini

68 Tena mwisho wao ni Motoni. Wao watakuwa katika adhabu ya milele. Wataletwa kutoka Motoni waje kula mti wa Zaqqum kisha wanyweshe kinywaji hicho, na tena warejeshwe mahala pao katika Jahannamu.