إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِزِينَةٍ ٱلۡكَوَاكِبِ ٦
Innā zayyannas-samā'ad-dunyā bizīnatinil-kawākib
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. 6
Maelezo ya chini
6 Sisi tumeipamba hii mbingu ya karibu na watu wa duniani kwa mapambo, nayo ni hizo nyota zinazong'ara, zenye ukubwa mbali mbali, na mwahala pao mbali mbali kwenye anga la ulimwengu kama ionekanavyo kwa macho.